Sunday, August 15, 2010

MTO SASIMO HATARINI KUTOWEKA

Picha hii inaonyesha Mto Sasimo unaoundwa na mito miwili.Mito hiyo ni Lengewaha na Mto Mlowa.

Mto Lengewaha unatumiwa na wananchi wa kitongoji cha Lengewaha kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo cha umwagiliaji maji kwa zaidi ya miaka 30.

Mto Sasimo nao unatumiwa na wananchi wa vijiji mbalimbali vya kata ya Malolo katika wilaya za Kilosa na Mpwawa kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji maji.

Kata ya Malolo ni eneo jangwa, ambalo halipati mvua za kutosha kwa mwaka na Mito inayotumiwa kwa shughuli za umwagiliajimaji ni Mto Mwega na mto Sasimo.Mazao makuu yanayolimwa katika eneo hili ni Kitunguu,Mpunga,Nyanya,Mahindi na Mbogamboga.

Pamoja na umuhimu wa mito hii kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Malolo na Lengewaha,Mito hii ipo katika hatari ya kutoweka kutokana na shuguli za kijamii zainazofanyika kwenye vyanzo vya mito hii.

Dalili za kuwepo kwa uwezekano wa mito hii kutoweka kabisa inatokana kupungua kwa mtiririko wa maji kwa kasi ambayo siyo ya kawaida.Lakini halii hii inasababishwa na nini?,

Uchnguzi wa mtandao huu umebaini kuwa chanzo cha kupungua kwa kasi kwa mito hii inatokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi wanaoishi katika kitongoji cha Lengewaha na milima ya kipengele mabako mto huu huanzi.

Uharibifu huo ni pamoja na Uchomaji moto msitu na kilimo ndani ya kingo za mito na kilimo cha vinyungu.

Ukweli ni kwamba kama hali hii itaendelea pasipo kuchukua hatua za makusudi kudhibiti hali hii ni dhahili kwamba siyo kitambo mito hii itatoweka kabisa licha ya umuhimu wake kijamii na kiuchumi.

Elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira katika maeneo haya inahitajika kuokoa mito hii kutoweka kabisa.

Kama uharibifu wa mazingira utaendelea kwa kasi hii,Kauli mbiu ya Kilimo kwanza itatekelezeka kwa vitendo?



No comments:

Post a Comment