Wakati hapo jana Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Bwana Lusiano Mbosa akimtangaza Dr.Mgimwa kuwa Mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo, huku akieleza kuwa lolote laweza kutokea kwa madai kuwa Dr.Mgimwa alikuwa akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kauli hiyo imegeuza upepo wa ushindi huo na kumuangukia Kandoro.
Akitangaza matokeo hayo hii leo katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bibi.Mary Tesha amesema matokeo yaliyotangazwa jana na kumpa ushindi Dr.Mgimwa haya kuwa sahihi na hivyo matokeo sahihi ni kwamba Abas Kandoro ndiye aliyeshinda kwa kura 5300 dhidi ya kura 5212 ambazo Dr.Mgimwa amepata.
Mtanado huu unaendelea kufuatilia uhalali wa matokeo haya kwani kunataarifa kuwa katibu kata wa CCM huko Ifunda anashikiliwa na polisi kwa kupokea hongo ya shilingi milioni tano kutoka kwa Abas kandoro kwa maelezo kwamba akubali kuwa alikosea kujumlisha matokeo hayo yaliyompa ushindi Dr.Mgimwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bwana Evarist mangala alipoulizwa kama jeshi lake linamshikilia katibu kata huyo amekanusha kuwa taarifa hizo hazija mfikia.
endelea kutembelea mtanadao huu ili kupata taarifa zaidi kuhusu sakata hili.

No comments:
Post a Comment