Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lyasa iliyopo wilaya ya Iringa wanaishi katika mazingira magumu ya kupanga uraiani katika nyumba ambazo hazina ubora kutokana na shule hiyo ya kata kutokuwa na mabweni.
Athari za kupanga uraiani pia zimesababisha wanafunzi sita wa kike katika shule hii kupata ujauzito na kuacha masomo lakini wengine wanadaiwa kuacha shule kutokana na utoro.
Kwamujibu wa wanafunzi hawa, maisha ya kupanga uraiani kunawaathiri kitaaluma kutokana na kazi mbalimbali ikiwemo kutafuta kuni msituni kwaajili ya kupikia na kujisomea kwa kutumia taa aina ya chemli.
Umbali kutoka shuleni hapo hadi kijijini kwao pia ni tatizo ambalo linaongeza machungu kwao katika harakati za kujikomboa kielimu kwani wakati wa likizo hulazimika kutembea umbali wa kilomita 12 hadi kufika nyumbani kwao kutokana na eneo hilo kutokuwa usafiri wa uhakika.
Mkuu wa shule hiyo Bwana Donard Kilundo amesema tatizo la kupanga uraiani linawakabili pia walimu wa shule hiyo kwani hadi sasa kuna nyumba moja tu ambayo ni ya mkuu wa shule.
Amesema wanafunzi hao wanalazimika kupanga katika nyumba za uraiani kutokana na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 400 kutokuwa na Mabweni.
Kutokana na ukubwa wa tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike, mkuu wa shule hiyo amesema imewalazimu kugeuza baadhi ya vyumba vya madarasa kuwa mabweni kuwanusuru wanafunzi wa kike kupewa ujauzito.
Sikiliza kilio cha wanafunzi hawa na mkuu wa shule hiyo katika video hii

No comments:
Post a Comment