Sunday, August 1, 2010

Habari zilizotufikia hivi punde

Habari zilizotufikia hivi punde kuhusiana na mchakato wa kura za maoni za kuteua wagombea wa ubunge na madiwani katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge ni kwamba katika jimbo la Iringa mjini ,aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Bwana Fredrick Mwakalebela amepitishwa kuwa mgombea wa ubunge kupitia CCM. Katika Jimbo la Kilolo,Prof.Msolla ameshinda kura za maoni. Lakini katika Jimbo la Mufindi Joseph Mungai ameangukia pua katika kura za maoni na huo ndio utakuwa mwisho wa JJ katika medani za siasa.

Endelea kutembela mtandao huu ili kupata matokeo zaidi katika majimbo mengine.

No comments:

Post a Comment