Monday, May 14, 2012

Na Lauria Mkumbata Iringa........Naibu waziri wa ujenzi Gerson Lwenge ametembelea sehemu ya nne ya  mradi wa ukarabati wa kipande cha barabara ya TANZAM kutoka Iringa hadi Mafinga chenye urefu wa kilomita 70.

Ukarabati wa barabara hiyo unatekelezwa na muunganiko wa makampuni ya Aasleff A/S kutoka nchini Dernmark na Interbeton BV ya Uholanzi kwa gharama ya Euro 38.5milioni.

Akiongea mara baada ya kukagua mradi huo Lwenge alisifu kampuni hizo kwa viwango na ubora wa kazi katika utekelezaji wa mradi huo.
Alisema barabara zinazojengwa na makampuni hayo ni miongoni mwa barabara zenye ubora wa viwangovya juu nchini kutokana na kuwa na alama zote muhimu za usalama barabarani.

Alitoa onyokali kwa Makandarasi wanozembea katika utekelezaji wa miradi ya barabara na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwafukuza kazi.

"Kama kuna mahali mkandarasi atazembe tutachukua hatua kali,lakini kama kazi ni mbaya tutachukua hatua kali kuanzia msimamizi wa mradi". alisisitiza.

 Mapema akieleza changamoto wanazokabiliana katika utekezaji wa mradi huo, meneja mradi wa kampuni ya Aasleff-Interbeton Wessel Schueting alizitaja kuwa ni pamoja na wizi wa vifaa vya ujenzi, pesa na mamlaka ya mapato nchini TRA kuchelewa kurudisha pesa ya msamaha wa kodi kwa wakati.

Kampuni ya Aasleff na Interbeton zimepewa kandarasi ya mradi wa ukarabati wa barabara hiyo baada ya kukamilisha kwa wakati mradi wa kwanza wa ukarabati wa barabara ya TANZAM kutoa iyovi hadi Iringa mjini.

 Utekelezaji wa mradi huo wenye urefu wa km 168 ulitekelezwa kwa gharama ya Euro 76.2milioni.

Naibu waziri wa ujenzi Gerson Lwenge katikati akipewa maelezo na Meneja mradi wa Kampuni ya Aasleff-Interbeton Bwana Wessel Schueting kushoto, kuhusu ujenzi wa barabara hiyo.
Ukandarasi ni Mitambo.
Moja ya mtambo wa kisasa unaotumika katika ujenzi wa Barabara.



Naibu waziri wa ujenzi Gerson Lwenge, kushoto akikagua ukarabati wa kipande cha Barabara ya TANZAM kutoka Iringa hadi Mafinga chenye urefu wa 70km.Kulia ni Bw. Wessel Schueting, meneja mradi wa kampuni ya Aarself-Interberton.

Mradi wa ukarabati wa barabara hii unagharim Euro milioni 38.5.na unatekelezwa na kampuni ya Aarself-Interberton.